Uturuki

Uturuki kuwa mwenyeji wa maonesho makubwa ya kimataifa kuhusu ulinzi Istanbul wiki ijayo

Maonesho hayo ya siku sita yanatarajiwa kuleta pamoja sekta ya ulinzi duniani katika maeneo mbalimbali kote jijini.

Newstimehub

Newstimehub

15 Julai, 2025

60471fd002ca3432fd6b39e3d33f8b84cdd3c573ba7554be3762ccf20adb5f8b

Moja ya maonesho makubwa ya masuala ya ulinzi duniani, Maonesho ya Kimataifa ya Ulinzi, yataanza wiki ijayo jijini Istanbul.

Maonesho hayo ya siku sita yataanza Julai 22 na yataandaliwa na Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Uturuki ikishirikiana na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki, sekta ya Ulinzi na Wakfu wa Jeshi.

Maonesho hayo ya 17 yatafanyika sanjari katika Kituo cha Maonesho cha Istanbul, Uwanja wa ndege wa Atatürk, Hoteli ya Wow na Atakoy Marina.

Maonesho hayo yataonesha magari ya kivita, magari yenye silaha ya kutumia mbinu vitani, magari ya ardhini yasiyo na dereva, vyombo vya angani, na baharini, mifumo ya silaha, roketi, makombora ya masafa marefu, silaha za kijeshi, michezo ya kijeshi, suluhu za kielektroniki vitani, vifaa vya kuondoa vilipuzi.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu, pamoja na kuwepo kwa hafla kadhaa za kutia saini makubaliano.

Maonesho yaliyopita yalifanyika Julai 2023 jijini Istanbul.