Marekani imetishia kuchukua hatua dhidi ya Rwanda, ikisema vitendo vyake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vinakiuka wazi makubaliano ya amani yaliyosainiwa Washington tarehe 4 Desemba. Kauli hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio inajiri huku Marekani ikiishutumu Rwanda kuchochea ukosefu wa utulivu kupitia kundi la waasi la M23—madai ambayo Kigali imekanusha—wakati juhudi za kidiplomasia za kumaliza mzozo huo zikiendelea kukabiliwa na changamoto.
CHANZO: TRT Afrika













