Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, imewahukumu kunyongwa hadi kufa maafisa watatu wa uhamiaji kwa kosa la kumuua Enos Elias, mkazi wa Kakonko, kwa madai kuwa hakuwa raia wa Tanzania. Mahakama ilibaini kuwa maafisa hao walitumia mateso na nguvu kupita kiasi licha ya ushahidi wa uraia wa marehemu kuwasilishwa na familia yake.
CHANZO: TRT Afrika













