Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa Mlango-Bahari wa Hormuz haujafungwa rasmi, lakini meli nyingi zinaogopa kupita kutokana na mvutano wa kijeshi unaoendelea katika eneo hilo.
Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X, alieleza kuwa kampuni za bima ndizo zinazosababisha taharuki kwa kuhofia hatari za vita vilivyochochewa na mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Licha ya hali hiyo, Iran imeonya kuwa meli zinazohusiana na mataifa yanayoshiriki vita zinaweza kuchukuliwa hatua kulingana na sheria na hali ya mzozo uliopo.
CHANZO: TRT Afrika














