Afrika

“Afrika inaweza kulisha dunia nzima,” asema Rais wa Senegal

Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, siku ya Jumatatu alisema kuwa Afrika inaweza kulisha dunia nzima, akisisitiza kuwa vijana lazima wawe kiini cha mageuzi ya kilimo.

Newstimehub

Newstimehub

2 Septemba, 2025

f50d12a52c3510840790d3ad17ea1422a12fd046ab9890f5f2bc836095f3037c

Rais Faye aliyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wa usalama wa chakula uliofanyika Dakar nchini Senegal na kuongeza kuwa, asilimia 65 ya ardhi inayofaa kwa kilimo duniani, na vijana wabunifu, na rasilimali nyingi ziko barani Afrika.

Rais Faye alihimiza Afrika ijitegemee yenyewe kufanikisha usalama wa chakula na kuchukua mtazamo wa kutafuta suluhisho, akisema hilo linahitaji uwekezaji mkubwa katika usimamizi wa maji, ubunifu, usindikaji wa mazao ndani ya nchi, na biashara kati ya nchi za Afrika.

Katika mkutano huo wa kila mwaka, Rais wa Rwanda Paul Kagame amelitaka bara la Afrika kuacha kutegemea dunia katika kila kitu na kusisitiza kwamba, bara hilo linaweza kujitegemea kwa sababu lina utajiri wa rasilimamali zote.