Serikali ya Afrika Kusini imesisitiza kuwa haitavunja uhusiano wake na Iran, licha ya kauli kutoka kwa balozi mpya wa Marekani kwamba uhusiano huo unadhoofisha mahusiano na Washington.
Afisa mkuu wa mahusiano ya kimataifa, Zane Dangor, alisema nchi yake haitajiingiza katika siasa za nguvu kubwa zinazoathiri uhuru wa maamuzi ya mataifa.
Aidha, alikataa masharti mengine kutoka Marekani, ikiwemo kuondoa kesi dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
Mahusiano kati ya Afrika Kusini na Marekani yamezorota tangu utawala wa Donald Trump, huku ushuru wa bidhaa kutoka Afrika Kusini ukiongezwa hadi asilimia 30.
CHANZO: TRT Afrika














