Aston Villa imeivunja rekodi ya Arsenal ya mechi 18 bila kupoteza baada ya kushinda 2-1 katika dakika za mwisho kwenye mchezo wa Premier League uliochezwa Villa Park. Matty Cash aliipa Villa uongozi kabla ya Leandro Trossard kusawazisha mapema kipindi cha pili.
Hata hivyo, katika dakika za mwisho kabisa, Emiliano Buendía aliifungia Villa bao la ushindi baada ya mtafaruku langoni, na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa nyumbani. Ushindi huo unaipandisha Aston Villa hadi nafasi ya pili, ikiwa pointi tatu tu nyuma ya vinara Arsenal, ambao wamepoteza kwa mara ya pili tu msimu huu.
CHANZO: TRT Afrika














