Polisi wa Australia wathibitisha kuwa wawili walioua watu 15 katika Ufuo wa Bondi walikuwa baba na mwanawe, Sajid Akram (50) na Naveed (24). Sajid alifariki papo hapo, huku mwanawe akiwa katika hali mbaya hospitalini. Duru za habari zinaarifu kwamba wawili hao waliapa utii kwa kundi la Islamic State, huku bendera za IS zikipatikana kwenye gari lao. Waathirika walihusisha watoto, wazee, na manusura wa Mauaji ya Kimbari. Waziri Mkuu wa New South Wales, Chris Minns, alitembelea hospitali huku Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese, akiahidi kushinikiza sheria kali za umiliki wa silaha. Sajid Akram alikuwa na leseni halali ya kumiliki silaha za moto kwa shughuli za uwindaji.
CHANZO: BBC NEWS





