Maonyesho makubwa ya ulinzi barani Afrika, BAMEX 2026, yanatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 9 hadi 13 katika mji mkuu wa Mali, Bamako.
Tukio hilo litawakutanisha wajumbe wa ngazi za juu na makampuni ya ulinzi kutoka nchi zote 54 za Afrika pamoja na washiriki kutoka mataifa mengine duniani.
Lengo kuu ni kuifanya Sahel, ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto za usalama, kuwa kitovu cha majadiliano na ubunifu katika sekta ya ulinzi.
CHANZO: TRT Afrika














