Rais wa Shirikisho la Soka nchini Congo (FECOFOOT), Jean-Guy Blaise Mayolas, amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya mahakama kumpata na hatia ya utakatishaji wa fedha zenye thamani ya dola milioni 1.3.
Katika kesi hiyo, Mayolas alishtakiwa pamoja na mkewe na mtoto wake kwa madai ya kutumia vibaya fedha zilizotolewa na FIFA. Fedha hizo zilikuwa sehemu ya ruzuku iliyotolewa kwa nchi wanachama kusaidia sekta ya soka wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.
Ruzuku hiyo ilikusudiwa kusaidia miradi ya maendeleo ya soka nchini Congo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya michezo na kuimarisha soka la wanawake.
Hata hivyo, wachunguzi walibaini kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zilitumika kwa maslahi binafsi ya Mayolas.
CHANZO: TRT Afrika














