Muungano wa nchi za Sahel—Mali, Niger na Burkina Faso—umelaani kutua kwa dharura kwa ndege ya kijeshi ya Nigeria aina ya C-130 katika mji wa Bobo Dioulasso, ukisema ndege hiyo ilikuwa na wanajeshi 11 na haikuwa na ruhusa ya kuruka katika anga yao. Muungano huo umelitaja tukio hilo kama “sio la kirafiki” na kutishia kuchukua hatua ya pamoja dhidi ya ukiukaji wowote wa sheria za anga. Haijafahamika hatma ya wanajeshi waliokuwemo ndani ya ndege hiyo. Nchi hizo tatu, ambazo zinapambana na makundi ya kigaidi, zimekuwa na mvutano na majirani zao wa Afrika Magharibi tangu kujiondoa ECOWAS na kuimarisha ushirikiano wao, huku pia zikiondoa uhusiano wa karibu na nchi za Magharibi na kugeukia Urusi.
CHANZO: TRT Afrika














