Afrika

Cyril Ramaphosa amsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Usalama ya Afrika Kusini

Kusimamishwa kwa Fazel kunakuja katikati ya sakata la tuhuma mbalimbali zinazolikabili jeshi la polisi la nchi hiyo pamoja na idara ya usalama hususani zile zinazomkabili kamishna wa Polisi wa eneo la KwaZulu-Natal, Nhlanhla Mkhwanazi mwezi Julai.

Newstimehub

Newstimehub

16 Oktoba, 2025

cb2d70b11cb16437bda72b9f9448c6362cb76267fad4df4cb5886a255b383d8c

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemsimamisha Mkuu wa Idara ya Usalama nchini humo Imtiaz Fazel, kupisha uchunguzi kuhusiana na utendaji wake wa kazi.

Katika taarifa iliyotolewa Oktoba 15, kamati maalumu bunge la nchi hiyo, yenye kushughulikia masuala ya intelijensia , imesema kuwa ilimtaarifu Rais Ramaphosa kuwa ilipokea malalamiko juu ya mwenendo wa Fazel.

Hata hivyo, kamati hiyo haikuweza wazi makosa yanayomkabili mkuu huyo wa Idara ya Upelelezi nchini humo.

Kusimamishwa kwa Fazel kunakuja katikati ya sakata la tuhuma mbalimbali zinazolikabili jeshi la polisi la nchi hiyo pamoja na idara ya usalama hususani zile zinazomkabili kamishna wa Polisi katika eneo la KwaZulu-Natal, Nhlanhla Mkhwanazi mwezi Julai mwaka huu.