Michezo

FIFA yafikiria kadi nyekundu kwa wachezaji wanaoziba midomo uwanjani

Hatua mpya inalenga kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika soka.

Newstimehub

Newstimehub

2 Mechi, 2026

444

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amesema kuna uwezekano wa kuanzishwa kwa adhabu kali dhidi ya wachezaji wanaoziba midomo wanapozungumza na wapinzani wao uwanjani.

Pendekezo hilo limejadiliwa baada ya kuongezeka kwa matukio ambapo wachezaji hufunika midomo yao wakati wa mazungumzo, jambo linalodaiwa kuficha maneno yanayoweza kuwa ya kibaguzi. Infantino alisema ikiwa mchezaji atafanya hivyo na kubainika ametumia lugha ya kibaguzi, anaweza kupewa kadi nyekundu moja kwa moja.

Suala hilo lilijadiliwa katika mkutano wa International Football Association Board (IFAB), ambao unasimamia sheria za mchezo wa soka duniani.

CHANZO: TRT Afrika