Afrika

Hamas warudisha mwili wa Mtanzania Joshua Loitu Mollel

Mwili wa Mollel ulikuwa ni sehemu ya miili mingine 22 iliyorudishwa kutoka kwa makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza, yaliyofikiwa Oktoba 10.

Newstimehub

Newstimehub

6 Novemba, 2025

424ee7c7a6bbb223cbb90ca2de8f8c74d7cc0ab65916ba02ab5ac2124ad7113c

Israel imesema kuwa kikundi cha Hamas kimerejesha mabaki ya aliyekuwa mwanafunzi wa Kitanzania, Joshua Loitu Mollel.

Mollel ambaye alikuwa anasomea kilimo nchini Israel, alichukuliwa kinguvu na kuuwawa wakati wa shambulio la Oktoba 7 katika eneo Kibbutz Nahal Oz.

Kikundi cha Hamas kinadaiwa kurudisha mwili wa Mollel siku ya Jumatano Novemba 5, 2025 ikiwa ni baada ya siku 761, kama sehemu ya mpango wa usitishwaji vita vya Gaza, ambao uliratibiwa na Rais Donald Trump wa Marekani.

“Baada ya kukamilika kwa shughuli ya utambuzi… wizara ya mambo ya nje imeijulisha familia ya mateka huyo kuwa mwili wa mpendwa wao umerejeshwa,” Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema.

Taarifa hizo, pia zilithibitishwa na jeshi la Israel.

Mwili wa Mollel ulikuwa ni sehemu ya miili mingine 22 iliyorudishwa kutoka kwa makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza, yaliyofikiwa Oktoba 10.

Kama sehemu ya mpango huo, Hamas ilikuwa ikiwashikilia mateka 48 mjini Gaza, huku 20 wakiwa hai na wengine 28 wakiwa wamekufa.