Wananchi nchini Tanzania wamejitokeza kwa wingi katika masoko na maduka makubwa kununua bidhaa muhimu kutokana na hofu ya kutokea machafuko tarehe 9 Desemba, siku ambayo maandamano yaliyopigwa marufuku yanatarajiwa kufanyika. Ripoti zinaonyesha foleni ndefu jijini Dar es Salaam na Mbeya, huku baadhi ya bidhaa kupanda bei au kuadimika. Serikali imeongeza doria za polisi na jeshi, ikihimiza utulivu na kuonya kuhusu hatari ya maandamano. Hofu hiyo imechochewa na kumbukumbu za ghasia za Oktoba 29 ambapo watu walikwama majumbani kwa siku kadhaa kutokana na ukosefu wa huduma.
CHANZO: BBC NEWS














