Mabingwa watetezi Ivory Coast wamemjumuisha tena Wilfried Zaha, 33, kwenye kikosi cha AFCON 2025 kitakachocheza dhidi ya Msumbiji, Cameroon na Gabon katika Kundi F. Zaha, anayekipiga Charlotte ya MLS, alikuwa nje ya timu tangu michuano ya mwaka jana ilipofanikiwa kutwaa ubingwa. Kocha Emerse Fae amesema wamehitaji wachezaji wazoefu na kuwekeza kwenye uwezo wa Zaha kuwabana mabeki. Zaha aliwahi kucheza England kabla ya kuchagua kuitumikia Ivory Coast.
CHANZO: TRT Afrika














