Afrika

Jeshi la Polisi Tanzania lakiri kumshikilia aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji Geofrey Mwambe

Kulingana na taarifa yake iliyotolewa Disemba 12, 2025, jeshi hilo limesema kuwa lilimkamata Mwambe Disemba 7, 2025 katika eneo la Tegeta wilaya ya Kinondoni.

Newstimehub

Newstimehub

12 Desemba, 2025

0b301ff956c9491c7783e572996de294f49b647f9d5ed72c408eca900b476b4f

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya limesema kuwa limemkamata na linaendelea kumshikilia aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji na Mbunge wa Masasi, Geofrey Mwambe kwa tuhuma za jinai ambazo zinachunguzwa.

Kulingana na taarifa yake iliyotolewa Disemba 12, 2025, jeshi hilo limesema kuwa lilimkamata Mwambe Disemba 7, 2025 katika eneo la Tegeta wilaya ya Kinondoni.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa Mwambe, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini humo (TIC), amekamatwa kwa tuhuma za makosa ya jinai.

“Hatua zaidi za kisheria zinakamilishwa,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Geoffrey Mwambe amewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara  kuanzia mwaka 2020 hadi 2021, akateuliwa tena kuwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), kuanzia mwaka 2021 hadi 2022.