Serikali ya Kenya imetangaza marufuku kwa raia wake kujiunga na jeshi la Urusi, ikionya kuwa hatua hiyo ni kinyume cha sheria na inaweza kuhatarisha maisha yao.
Maafisa wa serikali wamesema kuwa kumekuwa na taarifa za baadhi ya Wakenya kuvutiwa kujiunga na majeshi ya kigeni, hasa katika muktadha wa vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Serikali imeonya kuwa raia watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha, mamlaka zimehimiza wananchi kuwa waangalifu dhidi ya matangazo au ahadi za ajira zinazoweza kuwa za udanganyifu au hatari, zikisisitiza umuhimu wa kulinda usalama wa raia wake ndani na nje ya nchi.Chanzo: TRT Afrika














