Mamiau ya raia wa Somalia walikusanyika Jumapili mjini Mogadishu kupinga uamuzi wa Israel kuitambua Somaliland kama taifa huru. Waandamanaji walisisitiza kuwa Somalia ni taifa moja lisilogawanyika, wakisisitiza umoja na mamlaka ya nchi yao.
Wakiwa chini ya ulinzi mkali wa usalama, waandamanaji walieleza kuwa hakuna sehemu ya ardhi ya Somalia inayoweza kutambuliwa au kutolewa bila ridhaa ya taifa zima. Walitaja hatua ya Israel kuwa ukiukaji wa wazi wa uhuru na uadilifu wa eneo la Somalia.
Maandamano hayo yanajiri baada ya Israel kuwa nchi ya kwanza mwanachama wa Umoja wa Mataifa kutangaza rasmi kuitambua Somaliland, hatua iliyokosolewa na Somalia pamoja na mataifa kadhaa ya Afrika na Mashariki ya Kati.
CHANZO: TRT Afrika














