Senegal imefuzu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibwaga Misri 1-0 katika nusu fainali iliyochezwa mjini Tanger, Morocco. Bao pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 78 na nyota wa Al-Nassr, Sadio Mane, aliyepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Misri na kuwasha shangwe kubwa kwa mashabiki wa Senegal.
Misri, ikiongozwa na Mohamed Salah, haikuonyesha makali makubwa mbele ya lango la wapinzani. Kwa ushindi huu, Senegal—mabingwa wa AFCON 2021—wanatafuta taji lao la pili barani Afrika.
CHANZO: TRT Afrika














