Afrika

Mashirika ya ndege ya Qatar na Kenya kushirikiana

Qatar Airways na Kenya Airways wametia saini makubaliano yatakayowezesha abiria kusafiri katika maeneo mbalimbali duniani.

Newstimehub

Newstimehub

21 Oktoba, 2025

ef32608688fb93b817e9038180e5259d4ba23853ac4dc799bf1e2c2e4fead9f0

Mashirika ya ndege ya Qatar Airways na Kenya Airways yametangaza kuzindua mfumo wa ushirikiano utakawaofikisha wateja wao katika maeneo 19, huku maeneo mengine yakitarajiwa kuongezwa hivi karibuni.

Abiria wa Kenya Airways sasa wanaweza kuunganisha safari zao katika miji kumi kati ya Nairobi na Doha, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad.

Vilevile, wateja wa shirika la ndege la Qatar Airways wanaweza kufika katika maeneo nane kwa kutumia mtandao wa Kenya Airways, kutokana na safari tatu za ndege za kila siku kati ya Doha na Nairobi. Wateja wataweza kusafiri kwa kutumia mfumo huu kuanzia tarehe 26 Oktoba 2025.

Uuzaji wa tiketi kwa ajili ya safari hizo za ndege umeanza Jumanne 21 Oktoba.