Real Madrid imepunguza pengo dhidi ya Barcelona hadi pointi moja baada ya kuishinda Athletic Club 3-0 uwanjani San Mamés. Kylian Mbappé alifunga mabao mawili huku Eduardo Camavinga akitupia moja, katika mchezo uliotawaliwa na Los Blancos. Athletic walipata nafasi chache lakini Courtois aliokoa vyema. Hata hivyo, Madrid ilipata pigo baada ya Alexander-Arnold na Camavinga kuumia kipindi cha pili. Ushindi huu unaendeleza presha katika mbio za ubingwa wa La Liga.
Mbappé Aang’ara, Real Madrid Yawakaribia Barcelona Baada ya Ushindi Mnono Bilbao
Mbappé alitupia mabao mawili na kuiweka Real Madrid hatua moja karibu na vinara Barcelona.












