Mhifadhi mashuhuri wa tembo Afrika Mashariki, Iain Douglas-Hamilton, amefariki dunia jijini Nairobi akiwa na umri wa miaka 83. Douglas-Hamilton, aliyezaliwa Uingereza lakini kufanya kazi zake nyingi Uganda, Tanzania na Kenya, alitoa mchango mkubwa katika kupambana na ujangili wa tembo na alihusika katika juhudi zilizowezesha kupigwa marufuku kwa biashara ya pembe za ndovu. Taasisi ya Save the Elephants imesema kazi zake ziliweka misingi muhimu ya utafiti wa wanyamapori na zitakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika uhifadhi.
CHANZO: TRT Afrika














