Afrika Siasa

Miaka 5 Bila John Pombe Magufuli: Watanzania Waendelea Kumkumbuka

Leo ni miaka mitano tangu kifo cha aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania, huku wengi wakikumbuka mchango wake katika maendeleo na mapambano dhidi ya rushwa.

Newstimehub

Newstimehub

17 Mechi, 2026

491

Watanzania wanaadhimisha miaka mitano tangu kifo cha John Pombe Magufuli, aliyefariki Machi 17, 2021 katika jiji la Dar es Salaam kutokana na maradhi ya moyo.

Kiongozi huyo alijulikana kwa kauli mbiu yake ya “Hapa Kazi Tu” na juhudi zake za kusimamia nidhamu ya kazi serikalini pamoja na kupambana na ufisadi.

Katika uongozi wake, alianzisha mahakama maalum ya kushughulikia rushwa na kusukuma mbele miradi mikubwa ya maendeleo kama vile reli ya kisasa ya SGR na bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

Aidha, alifufua shirika la ndege la taifa (ATCL) na kusimamia ujenzi wa miundombinu mikubwa kama madaraja ya kisasa.

Hata hivyo, baadhi ya sera zake zilipingwa, hasa kuhusu uhuru wa kisiasa na vyombo vya habari.

CHANZO: TRT Afrika