Mkataba mpya wa ushirikiano wa afya kati ya Senegal na Marekani umeibua mjadala nchini humo, huku serikali ikijaribu kuwahakikishia wananchi kuwa makubaliano hayo yana lengo la kuboresha huduma za afya.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, mkataba huo unahusisha ushirikiano katika tafiti za kitabibu, kuboresha miundombinu ya afya, na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Hata hivyo, baadhi ya makundi ya kiraia yameonyesha wasiwasi kuhusu uwazi na masharti ya makubaliano hayo. Serikali ya Senegal imesisitiza kuwa makubaliano hayo yanalenga manufaa ya wananchi na kuimarisha mfumo wa afya wa taifa.
Chanzo: TRT Afrika














