Afrika

Mo Dewji Aendelea Kuwa Tajiri Zaidi Afrika Mashariki

Mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Dewji bado anaongoza utajiri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kulingana na orodha ya hivi karibuni ya Forbes.

Newstimehub

Newstimehub

11 Mechi, 2026

909feaae8ebfb57488e27ed6e38b966ecec84cd06885239a51de0c6ab0c65cdd e1773227796440

Mfanyabiashara maarufu wa Tanzania Mohammed Dewji, anayejulikana kama Mo Dewji, ameendelea kuwa tajiri zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati licha ya kushuka kwa nafasi mbili katika orodha ya matajiri barani Afrika.

Jarida la Forbes linaonyesha kuwa Dewji anashika nafasi ya 14 katika orodha ya matajiri wa Afrika, akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 2.1.

Katika orodha hiyo, mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote anaendelea kuongoza akiwa na utajiri wa dola bilioni 28.5, huku Johann Rupert na familia yake wakishika nafasi ya pili.

CHANZO: TRT Afrika