Timu ya taifa ya Morocco, maarufu kama Atlas Lions, imefuzu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibwaga Nigeria kwa penalti 4-2, kufuatia sare tasa ya dakika 120 katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat.
Kipa Yassine Bounou aling’aa kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti kutoka kwa Samuel Chukwueze na Bruno Onyemaechi, huku Hamza Igamane akiwa mchezaji pekee wa Morocco aliyekosa.
Morocco sasa itachuana na Senegal katika fainali Jumapili kwenye uwanja huo huo, ikilenga kutwaa taji mbele ya mashabiki wake wa nyumbani.
CHANZO: AA














