Kutokana na hatari inayoongezeka katika Mlango wa Hormuz, mamia ya meli za biashara na mafuta zimelazimika kubadili njia na kuzunguka Rasi ya Cape of Good Hope nchini Afrika Kusini ili kufika Ulaya.
Ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya meli 200 zimekaa nanga karibu na eneo hilo huku zingine zikielekeza safari zao kupitia Bahari ya Hindi na pwani ya Afrika Mashariki. Njia hiyo mpya inaongeza maelfu ya kilomita na kuchelewesha safari kwa takriban wiki mbili.
Wakati huo huo, baadhi ya meli za mafuta zimeripotiwa kuharibiwa katika eneo la Ghuba, jambo linaloongeza hofu kuhusu usalama wa biashara ya kimataifa na usambazaji wa nishati duniani.
CHANZO: TRT Afrika














