Afrika

Mwanaharakati na mjumbe wa amani Malala Yousafzai aitembelea Tanzania

Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel, yupo Tanzania akihimiza elimu kwa watoto wa kike.

Newstimehub

Newstimehub

11 Julai, 2025

6b58af4ff12a3624735d8ae32a4a98e5177a1347fe6f94e829fa79df0c4c49a3

Mwanaharakati wa mambo ya elimu na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, Malala Yousafzai yupo nchini Tanzania kwa shughuli maalumu ya kuhimiza elimu kwa watoto wa kike nchini humo.

Malala, ambaye alipokea tuzo ya amani ya Nobel, Oktoba 10, 2014, ameanza aliwasili nchini Tanzania, Julai 9, 2025 kama sehemu ya kampeni yake ya kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa ya elimu.

“Ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania. Nitakuwa nasherehekea siku ya Malala nikiwa katikati ya jamii za Watanzania, nikiwaunga mkono watoto wa kike wa Tanzania, nikipaza sauti zao na pia nikijifunza kutokana na mafanikio yao,” alisema Malala katika taarifa yake rasmi.

Kulingana na taarifa ilichapishwa kwenye tovuti ya taasisi ya Malala, katika ziara yake, mwanaharakati huyo anakutana na viongozi wa serikali, wadau wa elimu, hususani wale wanaohusika na elimu kwa mtoto wa kike na kujionea namna sanaa na michezo inavyotumuka kukuza elimu na uelewa ndani ya jamii za Tanzania.

 Mwaka 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha Julai 12 kama ‘Siku ya Malala’, ili kutambua jitihada zake za kuhakikisha wanafunzi wa kike wanapata fursa za elimu.

Azimio hili lilipitishwa baada ya mwanaharakati huyo kuponea jaribio la kuuwawa na kikundi Taliban wakati akirudi nyumbani kutokea shuleni, akiwa na umri wa 15 tu.