Afrika

Mwanamazingira Kijana Truphena Muthoni Apatiwa Tuzo ya Rais Ruto, Kenya Ipeperushwe Kimataifa

Truphena Muthoni, mwenye umri wa miaka 22, ametuzwa medali ya Head of State Commendation kwa juhudi zake za kuhifadhi miti na mazingira.

Newstimehub

Newstimehub

15 Desemba, 2025

146

Mwanamazingira Truphena Muthoni kutoka Kaunti ya Nyeri, Kenya, ametuzwa medali ya Head of State Commendation kutoka kwa Rais William Ruto kwa juhudi zake za kuhifadhi mazingira. Muthoni alijaribu na kufanikisha kukumbatia mti kwa saa 72, akiendelea na rekodi yake ya awali ya saa 48, huku akitarajia uthibitisho kutoka Guinness World Records. Rais Ruto alimtaja Muthoni kuwa balozi wa kampeni ya upanaji wa miti bilioni 15 nchini, na amesisitiza kwamba binti huyo atapata nafasi ya kushirikiana na wizara za utalii na uhifadhi wa wanyama pori kuhamasisha jamii. Kwa kuwa hakuweza kwenda Brazil kwa kongamano la COP 30, Muthoni alikamilisha jaribio lake la pili nchini Kenya, akiwa katika hafla iliyoambatana na mashangilio na pongezi kutoka kwa jamii na Gavana wa jimbo lake.

CHANZO: BBC NEWS