Afrika

Mwanamfalme wa Qatar ataka kuwekeza dola bilioni 21 DRC,serikali ya nchi hiyo imesema

Mwanamfalme wa Qatar Sheikh Mansour bin Jabr bin Jassim Al Thani anataka kuwekeza dola bilioni 21 nchini DRC, serikali ya nchi hiyo ilitangaza siku ya Jumatano.

Newstimehub

Newstimehub

3 Septemba, 2025

6d550b5d413b3632c2c9e72f5d67b054d1d18c3790221c861daf36cd5455e5fb

Shirika la uwekezaji la Al Mansour Holding linatarajia kuwekeza dola bilioni 21 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Qatar ni mpatanishi kwa lengo la kumaliza vita vya miaka mingi mashariki mwa nchi, serikali ya DRC ilitangaza siku ya Jumatano.

Mwanzilishi wa shirika hili na mmoja wa Wanamfalme Sheikh Mansour bin Jabr bin Jassim Al Thani alifanya ziara mji mkuu wa DRC, Kinshasa siku ya Jumanne ikiwa sehemu ya ziara yake ya bara la Afrika.

Ujumbe wa Qatar uliwasilisha ‘‘mapendekezo” ya kutaka kuwekeza karibu dola bilioni 21 nchini DRC wakati wa mkutano na Waziri Mkuu Judith Suminwa, ofisi yake ilisema katika taarifa.

Uwekezaji huo utakuwa katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, fedha, uchimbaji madini, dawa na haidrokaboni, iliongeza.

Kufanya ziara ‘ya kibinafsi’ DRC