Paris Saint-Germain (PSG) imefanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano ya Ulaya baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Monaco, na kushinda kwa jumla ya mabao 5-4 katika michezo miwili.
Monaco ndio waliokuwa wa kwanza kufunga kupitia Maghnes Akliouche kipindi cha kwanza, lakini mchezo uligeuka baada ya Mamadou Coulibaly kuoneshwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea vibaya Achraf Hakimi. PSG ilisawazisha kupitia Marquinhos kabla ya Khvicha Kvaratskhelia kuongeza bao la pili dakika ya 66.
CHANZO: TRT Afrika














