Afrika

Rais Museveni ataka serikali imiliki mtandao wa intaneti Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amependekeza kuwa Serikali lazima iwe na mamlaka juu ya mifumo ya msingi ya mtandao ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa bei nafuu.

Newstimehub

Newstimehub

4 Desemba, 2025

0f6d1c6db791e0a7399a3996e8f2a461051a858b33c50f02805ae54906d0018c main

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa miundombinu ya mtandao haipaswi kumilikiwa au kuendeshwa na makampuni ya binafsi, na kuongeza kusema kuwa udhibiti wa serikali ni muhimu ili kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma hiyo kwa raia.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Museveni alisema kuwa umiliki wa makampuni binafsi mara nyingi huongeza gharama kwani makampuni yanaendeshwa na faida badala ya maslahi ya taifa.

Kulingana na Rais Museveni, hali hiyo inafanya gharama za uunganishaji kwa raia kuwa kuwa ghali.

“Mtandao wa intaneti haupaswi kumilikiwa na watu binafsi…kwa sababu wakati mtandao unamilikiwa na wafanyabiashara, lengo lao ni kutafuta pesa, ndiyo maana unapaswa kumilikiwa na serikali.”

Alibainisha kuwa wakati watoa huduma wa kibinafsi wanachukua nafasi muhimu ya kutoa huduma, hawapaswi kudhibiti njia muhimu za usambazaji.

Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anagombea urais kwa muhula wa saba.