Afrika

Rais wa Somalia kufanya ziara rasmi nchini Uturuki siku ya Jumanne

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, atafanya ziara rasmi nchini Uturuki siku ya Jumanne, kwa mwaliko wa Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumanne na mkurugenzi wa mawasiliano wa nchi hiyo.

Newstimehub

Newstimehub

29 Desemba, 2025

32e5eb37d9ddc81acd177362bcc98124384db8feb43628fb010f782e21fa1ac1

Katika ziara hiyo Rais wa Uturuki na mwenzaka wa Somalia wanatarajiwa kujadili masuala kadhaa ikiwemo kutathminiwa kwa kina nyanja zote za ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

“Wakati wa mkutano huo, uhusiano wa mataifa mawili kati ya Uturuki na Somalia utatathminiwa kwa kina katika nyanja zote, na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuimarisha zaidi ushirikiano zitajadiliwa,” alisema Burhanettin Duran kupitia ukarasa wa mtandao wa kijamii wa Uturuki, NSosyal.

Mikutano hiyo pia itashughulikia maendeleo ya hivi karibuni katika mapambano ya Somalia dhidi ya ugaidi na juhudi za Serikali ya Somalia kuhakikisha umoja wa kitaifa, pamoja na masuala ya maendeleo ya kikanda.