Afrika

Rais wa Sudan Kusini aahidi kuboresha jeshi lake

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alimfuta kazi mkuu wa majeshi Paul Nang Majok 7 Julai 2025, baada ya kuwa kwenye nafasi hiyo kwa miezi saba tu na kumtaja mrithi wake Dau Aturjong Nyuol.

Newstimehub

Newstimehub

15 Julai, 2025

f4b2c147150b2923031e7a00d772066af29392d1d6298565b29f7e71d37933ad

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemwagiza Mkuu mpya wa Jeshi la Taifa la Sudan Kusini (SSPDF) Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Dau Aturjong Nyuol, kudumisha uadilifu, na kutoegemea upande wowote anapoongoza jeshi.

Rais Kiir ameahidi kufanya mageuzi yanayohitajika jeshini akiahidi kuunga mkono kikamilifu juhudi zinazolenga kulifanya jeshi hilo kuwa la kisasa zaidi.

“Wakati umefika wa kubadilisha jeshi letu la SSPDF kuwa jeshi la kitaalamu, umoja na la kisasa—lenye mafunzo ya kutosha, yenye vifaa vya kutosha, na lililojikita katika uzalendo na nidhamu,” Rais Kiir alisema katika hafla ya kumpa uongozi rasmi mkuu huyo wa jeshi.

Sherehe hiyo ilikuwa ya makabidhiano ya uongozi kutoka Mkuu wa zamani wa Majeshi Paul Nang Majok kwa Mkuu mpya Jenerali Dau Aturjong Nyuol.

Rais Kiir alisisitiza kuwa jeshi ni zaidi ya taasisi ya kijeshi.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alimfuta kazi mkuu wa majeshi 7 Julai 2025, baada ya kuwa kwenye nafasi hiyo kwa miezi saba tu na kumtaja mrithi wake Dau Aturjong Nyuol.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kumuondoa Paul Nang Majok.

Rais Kiir amemtaka Mkuu huyo wa Majeshi kuwa na ueledi na kuondoa siasa katika jeshi la taifa. Pia alisisitiza wito wa kuondolewa kwa “maafisa hewa” katika orodha ya wanajeshi wanaolipwa.

“Jeshi la SSDF ni ishara ya uhuru wetu, ngao ya uhuru wetu, na mlezi wa umoja wetu wa kitaifa, “Rais kiir alisema.