Senegal imesema itakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo baada ya CAF kubatilisha ushindi wake na kumpa Morocco taji la Kombe la Mataifa ya Afrika.
Uamuzi huo unakuja miezi miwili baada ya fainali iliyochezwa mjini Rabat kugubikwa na utata, ambapo wachezaji wa Senegal walitoka nje ya uwanja wakipinga penalti waliyopewa Morocco.
Licha ya kurejea na kushinda 1-0 kupitia bao la Pape Gueye, CAF iliamua kuwa Senegal ilikiuka kanuni kwa kuondoka uwanjani, na hivyo kuipa Morocco ushindi wa 3-0.
Shirikisho la Soka la Senegal limetaja uamuzi huo kuwa “usio wa haki na unaodhalilisha soka ya Afrika.”
CHANZO: TRT Afrika














