Seneti ya Nigeria imeidhinisha Rais Bola Tinubu kupeleka wanajeshi nchini Benin baada ya jaribio la mapinduzi lililoripotiwa Jumapili. Benin iliomba msaada wa haraka wa anga, na Nigeria ilituma ndege za kivita kuzuia wanajeshi waliokuwa wakijaribu kumwondoa Rais Patrice Talon. Hatua hiyo imechukuliwa kulinda utulivu wa kikanda, huku ECOWAS ikilaani jaribio hilo na kutangaza hali ya dharura Afrika Magharibi.
CHANZO: TRT Afrika














