Shabiki maarufu wa timu ya taifa ya DR Congo, Michel Kuka Mboladinga maarufu kama Lumumba Vea, atakosa kuhudhuria mechi ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kukosa visa ya kusafiri kwenda Mexico. DRC inatarajiwa kucheza dhidi ya Jamaica, lakini shabiki huyo atalazimika kubaki nyumbani huku akiendelea kuipa sapoti timu yake kwa mbali. Ameeleza kuwa ataendelea kuiunga mkono Leopards bila kujali umbali.
CHANZO: TRT Afrika














