Mtandao wa Madaktari wa Sudan umetangaza kuwa shambulio la droni lililofanywa na Rapid Support Forces (RSF) Jumapili usiku liliua watu watatu na kujeruhi saba katika hospitali ya Al-Mazmoum, jimbo la Sennar kusini mashariki mwa Sudan. Miongoni mwa majeruhi ni mfanyakazi wa afya.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa kushambulia taasisi za afya ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, ambazo zinakataza mashambulio dhidi ya vituo vya tiba na wahudumu wa afya. Mashambulio kama haya yanazidisha mateso ya raia na kuwanyima huduma muhimu za afya.
Kwa sasa RSF haijatoa majibu kwa tuhuma hizo.
CHANZO: AA














