Nyota wa soka wa Nigeria, Ahmed Musa, ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya karibu miaka 15 akilitumikia taifa. Musa anaondoka akiwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika historia ya Super Eagles, akiacha rekodi, mabao ya kihistoria ya Kombe la Dunia na kumbukumbu zisizofutika katika soka la Nigeria.
CHANZO: TRT Afrika












