Takriban watu kumi wamepoteza maisha katika ghasia zilizozuka usiku wa Ijumaa katikati mwa Uganda, muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais yaliyompa Rais Yoweri Museveni zaidi ya asilimia 75 ya kura. Mpinzani wake mkuu, mwanamuziki Bobi Wine, alipata takribani asilimia 21.
Ingawa siku ya upigaji kura ilifanyika kwa amani, vurugu zilianza katika mji wa Butambala, kilomita 55 kutoka Kampala, huku polisi na mbunge wa eneo hilo wakitoa maelezo yanayokinzana kuhusu chanzo cha mauaji.
CHANZO: TRT Afrika














