Afrika

Tanzania: Chama cha CCM kufanya mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge, viti maalumu

Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu ambao utahusisha mchakato wa kumchagua rais, wabunge, madiwani na wajumbe wa baraza la wawakilishi, Oktoba 29, 2025.

Newstimehub

Newstimehub

20 Agosti, 2025

1d41ee65582a510cb803f25b1050bb5d8f983aaf61916c84aa3a14eb009d4d86

Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha nchini Tanzania, kitafanya kikao cha siku mbili chenye lengo la kufanya teuzi za Wagombea Ubunge, wa Bunge la nchi hiyo, wabunge wa Viti Maalumu, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, anayeshughulikia itikadi, uenezi na mafunzo Amos Makalla, vikao hivyo ambavyo vitaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, vitafanyika Agosti 21 na 23, 2025 jijini Dodoma.