Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameoneshwa kushangazwa na baadhi ya watu waliotaka Rais Samia Suluhu Hassan asigombee urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akihoji kwanini hawakufanya hivyo kwa wakuu wa nchi wa serikali za awamu zilizopita.
Akizungumza Agosti 29, 2025, wakati wa uzinduzi wa kampeni za nchi nzima za chama hicho, zilizofanyika katika viwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam, Kikwete alidai kuwa wale wanaofanya hivyo, wanafanya kwa makusudi au wanajitoa ufahamu.
“Na mimi nililaumiwa kwa maneno niliyoyasema, na sasa nasema wanaotasema hayo ama wanajisahaulisha au wanajitoa ufahamu. Utaratibu wanaujua na walikuwepo,” alisema kiongozi huyo mstaafu.














