Wizara ya Afya ya Tanzania imetoa tahadhari kwa umma kutokana na ongezeko la maambukizi ya mafua na Uviko-19, huku ikisisitiza kuwa wagonjwa wengi ni wa hali hafifu na wanapona. Dkt Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Serikali, alisema hali inafuatiliwa kwa karibu kupitia vituo vya afya, vinavyohakikisha upatikanaji wa dawa muhimu, oksijeni na huduma za upimaji.
Wizara imesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuchukua hatua za kujikinga, ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka mikusanyiko, hasa kwa wazee, wajawazito na wagonjwa wenye magonjwa sugu.
CHANZO: TRT Afrika














