Ulimwengu Afrika

Marekani Yaweka Dhamana ya Dola 15,000 kwa Waombaji Visa Kutoka Nchi 50

Hatua mpya inalenga kupunguza wanaozidisha muda wa visa zao

Newstimehub

Newstimehub

18 Mechi, 2026

505

Utawala wa Rais Donald Trump umetangaza kuwa raia kutoka nchi 50 watalazimika kulipa dhamana ya dola 15,000 wanapoomba visa za kuingia Marekani. Hatua hiyo, itakayoanza Aprili 2, inalenga kuzuia wageni wanaozidisha muda wa kukaa nchini humo.

Mpango huo unahusisha visa za muda mfupi za biashara na utalii (B1/B2), na unahusu zaidi nchi za Afrika pamoja na mataifa mengine yaliyoongezwa hivi karibuni. Serikali ya Marekani imesema kuwa dhamana hiyo itarejeshwa iwapo mhusika atafuata masharti ya visa au hata kama hatasafiri kabisa.

CHANZO: TRT Afrika