katika taarifa kwa umma, tume imekuwa ikiwahimiza raia wa Kenya ambao wamefikisha umri wa kujisajili wafanye hivyo katika ofisi zozote za maeneo bunge, isipokuwa sehemu ambazo ziko kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo.
“Tume inawahimiza raia wote ambao hawajajisajili kuchukuwa fursa hii ya kushiriki mchakato unaondelea na kujisajili mapema,” IEBC ilisema.
Huduma za mchakato huu ni pamoja na usajili wa wapiga kura wapya, kuhakiki daftari la wapiga kura, wanaotaka kuhama vituo vya kupiga kura au maeneo bunge.
Ili kukidhi vigezo, lazima mtu awe raia wa Kenya aliyefikisha umri wa miaka 18, awe na kitambulisho cha taifa cha Kenya au pasi ya kusafiria, na awe hajasijajili awali, pamoja na kutopatika na hatia ya kuhusika na uhalifu wa masuala ya uchaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na awe na akili timamu.
Tume inasema inalenga kusajili wapiga kura wapya milioni 6.3 ambao walipata vitambulisho vya taifa katika miaka michache iliopita.














