Rais Yoweri Museveni amewaonya wapinzani akisema Uganda “sio nchi ya kuchezewa” wakati akihutubia viongozi wa mashinani wa NRM katika eneo la Lango. Alisisitiza kuwa NRM ndiyo imeleta amani tangu 1986 na kuonya wananchi kuwa makini na wanaoipinga serikali. Kauli hizi zinakuja kuelekea uchaguzi wa 2026, huku wapinzani wakimshutumu kwa ukandamizaji na ukiukaji wa haki.
CHANZO: TRT Afrika














