Serikali ya Ukraine imetoa onyo rasmi kwa raia wa Ghana dhidi ya kujiunga na majeshi ya Urusi yanayopigana vita nchini humo. Mamlaka zimesema watu wanaovutiwa na ajira au malipo wanapaswa kuwa makini kwani hali ya vita ni hatari na inaweza kuhatarisha maisha yao.
Pia imeelezwa kuwa kujiunga na vikosi vinavyoshiriki vita kunaweza kuwaletea athari za kisheria na kidiplomasia.
Chanzo: TRT Afrika














