Umoja wa Afrika (UA) umelaani vikali shambulio la risasi lililotokea katika ufukwe wa Bondi, Sydney, ambalo liliua angalau watu 16 na kujeruhi wengine takriban 40. Mwenyekiti wa Tume ya UA, Mahmoud Ali Youssouf, amelielezea tukio hilo kuwa ni kitendo cha kigaidi kinachokiuka maadili ya ubinadamu, amani na mshikamano wa kijamii. UA pia imetoa rambirambi kwa familia za waathirika na kuonyesha mshikamano wake na Australia, huku ikitoa wito wa ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na chuki, vurugu na misimamo mikali. Serikali ya Australia imesema shambulio hilo lililenga raia wa Kiyahudi waliokuwa wakisherehekea Hanukkah.
CHANZO: TRT Afrika














