UNICEF imesema mlipuko wa kipindupindu DR Congo umeua karibu watu 2,000 tangu Januari, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 340 watoto. Zaidi ya kesi 64,000 zimeripotiwa katika mikoa 17, huku ukosefu wa maji safi na usafi wa mazingira ukiongeza kasi ya maambukizi. Shirika hilo limeomba ufadhili wa dharura ili kuzuia vifo zaidi.
CHANZO: BBC NEWS














